Gaza: Gereza la watu milioni 1.5
Izrael, Februari 2006, siku moja baada ya uchaguzi wa Palestina, Izrael ilianza kuiwekea mlolongo wa vikwazo vya kisiasa na kiuchumi Gaza.  Toka mwaka 2007, Vikwazo hivi vimeongezwa ugumu.  Anga, ardhi na vizuizi vya bahari viliwekwa Gaza.  Mipaka ya kuingia na kutoka kwa binadamu na bidhaa  viliwekwa.  Tangu Desemba 2008 hadi Januari 2009 kwa siku 22 mfululizo kutokana na Operesheni ya Mimina Risasi  vyanzo vyote vya maisha vimekauka Gaza, ardhi ya kilimo, mashule, sehemu za kazi na makazi ziliharibiwa.


Hadi Sasa, milioni 1.5 ya wapalestina Gaza wanahangaika kuendeleza maisha yao katika jela ya wazi.  Asilimia  72 ya watu wa Gaza wanaishi katika njaa, kati yao asilimia 65 ni watoto.  Aslimia 10 ya watoto hawakui kimwili. Umoja wa mataifa hufafanua kama hali “tete”.

 

Imani ya dunia ilikutana katika meli hii
Mei 2010 tarehe 6 shirika la kimataifa lisilo la kiserekali, İHH Wakfu ya Msaada kwa Binadamu, harakati za Gaza huru, kampeni za nchi za ulaya kuondoa vikwazo Gaza, meli kwenda Gaza, Ugiriki, meli kwenda Gaza, Swideni na kamati ya kimataifa ya kuondoa vikwazo juu ya Gaza- michango iliyokusanywa takriban tani 6000 ya msaada kwa binadamu, ili kufikisha Gaza meli ya misaada iliundwa.  Pamoja na misaada ya kibinadamu meli ilibeba wanaharakati 750. wanaharakati kutoka katika nchi 37, nchi kama Ujerumani, Kuweit, Izrael, Ireland, Swiden, Ugiriki, Kibris ya kusini, Moroko, Yemen, Misri na Aljeria kati yao wabunge 15, takriban wanahabari wa kimataifa 60, wasanii na wanaharakati waliowahi kupata tuzo ya Nobel pia walikuwemo.

 

Izrael iliwapiga raia
Mei 30, meli 6- Defne, Gazze l, Eleftheri Mesogios, Sfendoni, Challenger 1 na Mavi Marmara-zilikutana katika uwazi wa kisiwa cha Kibris.  Mei 31 asubuhi meli ilikuwa imeshika njia ya kwenda Gaza moja kwa moja huku zikiwa zimezungukwa na jeshi la Izrael meli kubwa za kivita 4, helikopta 3, nyambizi 2 na meli ndogo za kivita 30 ziliwazunguka.  Asubuhi saa 10:32 katika maji ya kimataifa umbali wa maili 73 kutoka katika fukwe ya Gaza, wanajeshi waliosheheni vifaa huku wakipiga risasi waliingia katika meli ya Mavi Marmara ambayo iliyokuwa ikiongoza safari; wanajeshi wakitumia risasi za plastik na za moto waliwalenga raia. Raia wa Uturuki 8, mturuki-mwamerika 1 wanaharakati 9 wakusaidia binadamu wasio na silaha waliuwawa, watu 56 walijeruhiwa vibaya.  Matangazo ya moja kwa moja kutoka kwenye meli yalikatwa, lakini jeshi la Izrael walishindwa kutambua na matangazo yaliendelea kurushwa moja kwa moja bendi ya pili na dunia yote ilishuhudia mashambilio ya kinyama ya Izrael.


Wanaharakati wote walitolewa hadi katika sehemu ya wazi, mikono yao ikiwa imefungwa; hawakupewa chakula wala maji, hawakupewa ruhusa ya kwenda msalani, vitu vyao binafsi vilizuiliwa.  licha ya wanaharakati 750 kuwekwa kizuizini bila ya ridhaa yao, walikamatwa kwa kuingia Izrael bila ya idhini.  Meli zilivyutwa kwenda kwenye bandari ya Ashdod karibu na Tel Aviv.  Wanaharakati walishushwa kutoka kwenye meli mojamoja wakiongozana na polisi mojamoja huku wamefungwa pingu.  Hapa abiria wote kwa kuvuliwa nguo walisachiwa mara nyingi.  Wote chini ya ulinzi mkali, walipigwa picha na kuchukuliwa alama za vidole, rikodi ya macho yao ilichukuliwa na waliwekwa kwenye maulizo, muda mfupi baadae wanaharakati wote walipelekwa katika gereza la Beer-Sheva.  Hawakupewa idhini ya kuzungumza baina ya wao kwa wao au kupiga simu nchi nje.


Kutokana na shinikizo kubwa ya kidiplomasia ya kimataifa wanaharakati waliachiwa baada ya siku 2.


Huu ni muhtasari wa yaliotokea katika meli ya Mavi Marmara na yaliotekea Palestina usiku wa Mei 31.  Kuishi katika vurugu ya kisaikolojia na kimwili, kuwekwa kizuini kwa nguvu, kutekwa, kukamatwa, kudhuriwa, kuachwa na njaa, kutopata habari kutoka kwa mtu yoyote, kutoweza kutoa habari kwa mtu yoyote, kuuliwa...


Watu wa palestina wanaishi hivi kwa miaka 63.